Ads (728x90)

Tabs

Page

maxresdefault
NYOKA ni mojawapo kati ya viumbe hatari zaidi kwa viumbe wanaotambaa.
Lakini si kila nyoka ana hatari kama ya nyoka mwingine, leo katika chimbo la papaso tunamtazama nyoka aendaye kwa jina la BLACK MAMBA.


BLACK MAMBA jina lake hili halitokani na rangi ya ngozi yake bali rangi ya ulimi wake, huyu ndiye nyoka pekee ambaye ana ulimi na kinywa cheusi kwa ujumla.
Black mamba ni nyoka mwenye hatari zaidi kupita wote barani Afrika.
Tone moja tu la sumu iliyo katika kinywa cha Black mamba linatosha kabisa kumuua mwanadamu mtu mzima, na wakati wote anakuwa na matone ishirini katika kinywa chake, hivyo Black mamba anao uwezo wa kuua wanadamu watu wazima 20 kwa mapigo ya kufuatana.
Nyoka huyu ndiye nyoka mwenye mwendokasi mkali kupita nyoka wote na ndiye nyoka mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri kuliko nyoka wote.
Black mamba anakimbia umbali wa maili 12 kwa saa moja tu!!

Wakati nyoka wengine wakiwa wanavuka barabara ni rahisi kugongwa na gari ama pikipiki lakini Black mamba hujileta barabarani kwa sababu maalumu. Yeye huja kuwinda, kutokana na kuwa na speed kali ana uwezo wa kurukia windo lake na kulidhuru upesi. Hivyo unashauriwa kuwa ukimuona Black mamba barabarani ni heri usimamishe gari kuliko kumfuata.
Maajabu mengine ya nyoka huyu ni kwamba anaweza kukimbia kwa kasi huku robo tatu ya mwili wake ukiwa umesimama. Hii inamuwezesha kuweza kuliona windo lake vizuri zaidi…
Sumu ya Black mamba ni hatari sana, hushambulia moyo na upande wa ubongo, hivyo mtu aliyeumwa na nyoka huyu hurukwa na akili.
Wakati nyoka wengine mpaka wakasirike ndio sumu hupanda mdomoni, kwa black mamba ni tofauti kila wakati sumu ipo katika kinywa chake.
Sumu ya black mamba humuua mwanadamu kwa dakika zisizozidi 20

Wakati viumbe wengine hujali kuhusu uzazi wao hasahasa watoto wao, Black mamba jike hutaga mayai kumi na tano hadi ishirini na tatu kwa awamu moja, na akimaliza kutaga habari inaishia hapo harudi kamwe kutazama maendekeo ya mayai hadi yatakapojitotoa yenyewe.
Kinda la Black mamba punde linapotoka katika yai lina sumu mdomoni ambayo inaweza kumuua mwanadamu.
Ukisikia mtoto wa nyoka ni nyoka basi ndio hii!!
Kinda linajitotoa likiwa na urefu wa sentimita hamsini na moja. Hukomaa zaidi hadi kufikia urefu wa mita mbili na nusu.
Black mamba anayeshikilia rekodi ya kuwa mrefu zaidi aligundulika huko Zimbabwe akiwa na urefu wa mita nne…..

Black mamba anaishi hadi miaka 12!!!!

**Naam! Huyo ndiye Black mamba, nyoka hawa wanapatikana sana Swaziland na kwa Tanzania wanapatikana zaidi Tabora… japokuwa popote pale wanaweza kuwepo….

Post a Comment