Kulikuwa
na mfululizo wa uvamizi wa Vituo vya Polisi, watu wakapata hofu wengine
walihusisha matukio hayo na ishu ya ugaidi baadae hali ikawa sawa.
Matukio hayajaisha, nimeipokea ripoti ya
ITV kutoka
Morogoro inayohusu watu watatu kufariki katika mapambano na Polisi,
huku wawili kati yao wakihisiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la
Al Shabaab.
Breaking News nyingine kuhusu tukio hilihili iliyoripotiwa na Gazeti la Mwananchi inahusu
watu sita kukamatwa na wengine 50 wanatafutwa, walikutwa wakiwa na sare
za majeshi pamoja na silaha kama majambia kwenye msitu Mvomero.
Kwenye taarifa iliyofatia kutoka
Mwananchi, imesema Mkulima Cassian Peter amefariki mchana wa June 27
2015 kwenye Hospitali ya Bwagala ambapo Polisi mmoja amelazwa na hii ni
baada ya kujeruhiwa na hao watuhumiwa wa Ugaidi kabla hawajakamatwa.
Mtangazaji na Mwandishi wa habari wa Radio One Maulid Kambaya kwenye page yake ya Facebook alipost picha za walivyokamatwa navyo ‘Magaidi’ hawa.
Post a Comment