Ads (728x90)

Tabs

Page

maiti kenyaKifo
ni njia ya kila mmoja lakini watu wengi huogopa mtu aliekufa kutokana
na hilo utakubaliana na mimi kuwa kunahitajika ujasiri wa aina yake kwa
mtu kufanya kazi ambayo itamfanya kukutana na
watu waliokufa kila siku.
Mwanamke mmoja nchini Kenya Magreth Wanjiru ambae
ni mhudumu kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Nyeri
ameonekana kuwa mwanamke mwenye ujasiri wa hali ya juu, kutokana na
kufanyakazi ya kusafisha maiti na kuziweka dawa kazi ambayo anaifanya
kwa muda wa miaka miwili.
Magreti amesema kuwa aliamua kujifunza kazi hiyo baada ya mama yake
kufariki, ujasiri alioupata  kutokana na safari nyingi za kufika
Hospitali  kumuona mama yake aliyeugua kwa muda mrefu na kumfanya asiwe
na uwoga wa watu waliokufa.
Hata hivyo amepinga dhana kuwa mtu anaefanya kazi hiyo lazima awe
anatumia kilevi au dawa za kulevya kazi inayoaminika kuwa inafanywa na
wanaume pekee.

Post a Comment