Haya Ndio Makubwa Yaliyomkuta P.Diddy.
Multi-millionea na HipHop superstar P Diddy ameingia kwenye headlines za leo baada ya kujikuta matatani na polisi kwa kosa la kumshambulia kocha wa mpira katika mazoezi ya mechi ya mpira ya mwanae katika chuo cha UCLA.
Msanii huyo alikamatwa kwenye majira ya saa sita na nusu mchana kwenye maeneo ya Acosta Athletic Training Complex, na kufunguliwa file la makosa hayo, japo hakuna mtu yoyote aliumia P Diddy aliweka selo kuanzia saa sita hadi saa kumi na mbili na kuachiliwa baada ya kushindwa kupata kisa kamili cha kwa nini shambulio hilo lilitokea.
Lakini licha ya P Diddy kuachiliwa, polisi wamesma milionea huyo alitakiwa kufikishwa jijini Los Angeles kwenye County Sheriff’s Department Inmate Reception Center na bado mipango hio inaendelea.
Post a Comment