Teknolojia inatufungulia mapya kila siku.. Nakumbuka simu za kwanza
za mkononi zilikuwa kubwa halafu nzito, baadae ikaja fashion ya simu
ndogo ndogo, zile kubwa watu wakawa wanaziita ‘mshindi’ ambalo ni jina
la sabuni… Sasa hivi tunaona fashion ya simu kubwa
inarudi mdogomdogo.
inarudi mdogomdogo.
Sean Miles anaingia kwenye historia, anaingia kwenye headlines pia..
yeye kagundua hii simu ambayo imetengenezwa kwa majani kabisa pamoja na
mchanganyiko wa vitu vingine vilivyochakaa ama vilivyoharibika.
Dili
ambayo alipewa na Kampuni ya O2 ilikuwa Miles afanye ubunifu njia
ambayo wataweza kutumia mabaki ya vitu ambavyo vimechakaa na havifai kwa
matumizi, katoka na hii ambayo hata waliomuagiza hiyo kazi
imewashangaza yani.
Unaambiwa cover ya simu hii ukiiangalia ni kama majani kabisa.
Ubunifu
huu umefungua ukurasa mpya kwenye Teknolojia, Kampuni ya O2 wanaangalia
kama wataweza kuweka nguvu nyingi zaidi ili simu zenye cover hizi
zilizotengenezewa majani zitengenezwe nyingi na kuingia kwenye soko la
Dunia.
Vipi mtu wangu ukikutana na hii simu pale Kariakoo an Mlimani City kuna kitu kitakufanya usiipende labda?
Post a Comment