Najua kuna watu wangu ambao wanatamani sana siku moja wapate angalau dakika tano tu za kuchill na mastaa wanaowapenda na kupiga nao stori mbili tatu au hata kupata bahati tu ya kupiga nao selfie roho zao ziridhike yani. Ila umeshawahi kusikia stori za vituko vya mashabiki vikihadithiwa na mastaa?
Nimekutana na interview moja alioifanya msanii Trey Songz akihadithia vituko vya mashabiki anavyokutana navyo akiwa ana fanya shows mbali mbali Marekani, lakini vituko hivi viwili kwake ndio vimevunja rekodi na amesema hawezi kuja kuvisahau.
TS >>>“kuna kipindi nilienda Chicago bwana kupiga show, nikalipia chumba fulani hivi cha bei poa wala sikutaka makuu. Sasa kile chumba kilikua kina milango miwili, mlango wa kwanza ulikua unakuleta kama kwenye ki-reception fulani alafu mlango wa pili ndio ulikua unaelekea chumbani kwangu. So siku hiyo bwana baada ya kupiga show nikarudi hotelini kwangu, sina habari wala nini kaka wa watu nikafika mwenyewe, sasa nilivyo fungua mlango na kuingia tu nikakutana na vichwa wawili vilivyonishitua vikichungulia nyuma ya counter huku wamebanana na mwengine mmoja alikua amejibana nyuma ya mlango! ile naingia tu…washikaji wakanivamia kila mmoja ananivuta upande wake. Sikujua walitoka wapi na waliingiaje chumbani changu, sijui walipanda madirisha,yani mpaka leo sielewi…ila ile kitu walijipanga sana, sidhani hata kama walikuepo kwenye show wale!”
TS >>>“Aaah wadada bwana, hao ni shida! kuna huyo mmoja bwana yeye akaona isiwe tabu eti kukaa kusubiria autograph yangu kwenye foleni? aliona sio ishu! Yule dada bwana alipanda zile ngazi zinazo fungwa ukutani nyuma ya haya majengo marefu mpaka kufikia dirisha la chumbani changu gorofa ya tatu huko, sasa mimi nimefika chumbani nataka niingie bafuni nasikia mtu anapiga dirisha, kufungua pazia nakuta mtu ana ninginia dirishani kwangu, yani nilishituka alafu nikawaza kapigaje mahesabu na kujua nitakua naingia chumbani muda huu!! Nikafungua dirisha na kumsaidia aingie ndani manake niliogopa sija akadondoka alafu akaumia au akafa alafu ikawa stori nyingine. Alivyoingia ikabidi nimkumbatie manake kazi aliofianya haikua ndogo, nikapiga nae picha alafu nikawapigia simu security waje wamchkue, kituko hiki nacho kilintokea hotelini pia!”
Post a Comment