Ona Mama na mtoto wake walivyopona kwenye ajali ya ndege Colombia.
Kuna ajali ikitokea alafu unaambiwa wapo watu waliotoka wazima, inakuwa stori ya kushtua watu wengi sana, tena ajali yenyewe unaambiwa ni ya ndege!
Ndege bado ni usafiri salama duniani lakini ajali zake huwa mbaya pia, na ni mara chache kukuta imetokea ajali alafu wapo waliopona.. ajali ya ndege imetokea
Jimbo la Choco, Colombia siku tano zilizopita, leo ishu iliyo kwenye headlines inahusu mama mmoja na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja ambao walikuwemo ndani ya ndege iliyopata ajali na wametoka hai!
Mama wa mtoto huyo Maria Nelly Murillo amekutwa akiwa na majeraha madogomadogo pamoja na alama za kuungua, lakini mtoto amekutwa salama kabisa!
Wahusika wa Kitengo cha kuongozea ndege wanasema ndege ilipata ajali baada ya kupoteza mawasiliano kama kwa dakika 20 hivi, walianza kuitafuta na baada ya siku mbili wakakuta mabaki ya ndege kwenye msitu mkubwa… kupona kwao ni kama bahati tu, haijawekwa idadi kamili ya watu waliokuwemo kwenye ndege ila rubani Carlos Mario Ceballos nae alikutwa amefariki.
Maria amesema baada ya ajali alifanikiwa kufungua mlango wa ndege na kukimbilia kwenye msitu wakati huo ndege ilianza kuwaka moto tayari.. ndani ya ndege kulikuwa na samaki pamoja na nazi, mwanamke huyo aliweza kuishi siku zote hizo kwa kunywa maji ya nazi pekeyake.
Post a Comment