Unajua ukizitaja nchi ambazo zimekuwa
zikizungumziwa sana kuwa na sheria ngumu na kali, China nayo imo…
unaweza kuona ishu ya kukamatwa unawinda ndege ni kesi ndogo lakini sio
kesi ndogo kwa Wachina.
Vijana wawili ambao ni wanafunzi wa Chuo
wamejikuta kwenye mikono ya Mahakama na kesi ya kujibu kwa tuhuma za
kuwinda ndege ambao wamo kwenye list ya viumbe vilivyo hatarini
kutoweka.
Kesi yao ilikuwa kwenye Mahakama ya Huixian county na hukumu kutoka Mahakamani hapo inasomeka hivi; kila mmoja wao amepigwa faini ambayo ni sawa na Tshs. Mil.3.2 kwa kosa la kuwinda ndege hao na pia kuwauza, na mwisho wa yote ni kifungo cha miaka 10 na miezi sita kila mmoja jela.
Jamaa walinaswa baada ya kuwinda ndege
hao 12, mmoja alikufa mwingine akatoroka.. wengine 10 waliwauza kwa njia
ya mtandao ambapo jumla ya pesa waliyopata inagusa kama laki tatu na
nusu tu !!..
Post a Comment