Stori kutoka mtandao wa mirror.co.uk zinataja kuwa kocha wa klabu ya Real Madrid ya Hispania Rafael Benitez hatolalamika wala kuchangia chochote kama Real Madrid wataamua kumuuza Ronaldo, hizi ni stori za uchunguzi ambazo pia zinadhiirisha kuwa wawili hao hawapo vizuri kwani kwa nyota kama Ronaldo kuondoka katika klabu fulani na kocha wake akubali kirahisi huwa ni ngumu sana.
Benitez anaelewa kuwa Rais wa Real Madrid Florentino Perez yupo katika presha ya kifedha ya uchaguzi wa kutaka kuwania awamu nyingine, hivyo lolote linaweza kutokea, Ronaldo amekuwa akihusishwa kwa siku za hivi karibuni kuwa na mpango wa kurudi Man United au kutimkia klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa.
Post a Comment