Usiku wa November 28 mshambuliaji wa Leicester City Jamie Richard Vardy aliingia katika headlines baada ya kutumia dakika 24 za mwanzo za mchezo kati ya Leicester City dhidi ya Man United kuvunja rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Man United muholanzi Ruud van Nistelrooy ya kuongoza ufungaji magoli mfululizo.
Ruud van Nistelrooy ambaye aliondoka Man United mwaka 2006 na kujiunga na Real Madrid ya Hispania
aliweka rekodi ya ufungaji magoli 10 katika mechi 10 mfululizo, rekodi
ambayo imedumu kwa miaka 12 na usiku wa November 28 ndio mshambuliaji
raia wa Uingereza Jamie Richard Vardy aliivunja rekodi hiyo dakika ya 24 ya mchezo dhidi ya Man United.
Naomba nikusogezee list ya majina 23 ya wanasoka ambao wanaongoza kwa ufungaji magoli mfululizo katika Ligi Kuu Uingereza ila kwa sasa Jamie Richard Vardy ndio anaongoza kwa kuwa namba moja.
Hii ni sehemu ya video ya magoli bora ya Ruud van Nistelrooy
Post a Comment