Uwanja wa Stamford Bridge ni moja ya
viwanja maarufu duniani katika mchezo wa soka, huu uwanja unamilikiwa
na vigogo wa soka Chelsea.
Uongozi wa klabu hiyo tayari
umewasilisha maombi ya mpango wake wa kupanua uwanja wao ili uweze
kuingiza mashabiki 60,000 kwa wakati mmoja.
Pamoja na maombi hayo tayari
manispaa ya London Borough of Hammersmith na Fulham imekaribisha maoni
toka kwa wananchi ili watoe ridhaa yao au pingamizi kabla ya kuruhusu
upanuzi wa uwanja huo ambao utalazimu kubomoa baadhi ya majengo yaliyo
karibu na uwanja huo.
Chelsea, walianza kutumia uwanja wa Stamford Bridge, tangu 1905
ambapo mara ya mwisho kukarabatiwa na kupanuliwa ilikua mwaka 1990 na
kuufanya uwe na uwezo wa kuchukua watazamaji 42,000.Endapo ujenzi huo utaanza utamalizika mwaka 202o na utatumia kiasi ya Euro milioni 600.
Post a Comment