Muimbaji wa Nigeria Wizkid anatarajia kufanya show kwenye jukwa moja na msanii Alicia Keys na mchekeshaji Chris Rock.
Blogs za Nigeria zinasema hii ni kutokana na ukubwa wa wimbo wake wa
Ojuelegba Remix Ft Drake uliopata umaarufu mkubwa nje na ndani ya
Africa.
Wizkid atafanya show kwenye hafla ya 12 ya kuchangisha pesa za kampeni ya Keep a Child Alive inayosimamiwa na Alicia Keys.
Kama hufahamu kampeni ya Keep a Child Alive ilianzishwa na Alicia
Keys 2003 ikiwa ni kampeni kubwa duniani ya kupunguza maambukizi ya
virusi vya Ukimwi kwa watoto.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment