Ads (728x90)

Tabs

Page



Tukiwa bado tuko kwenye headlines za Uchaguzi zimebaki siku 5 za mtanzania kufanya maamuzi ya kumchagua kiongozi wake, sasa leo nakusogezea hii stori kutokea Tume ya Uchaguzi kuhusu kitambulisho cha kupigia kura.
Kwa kifupi niseme kwanza ni kinyume na taratibu ile kadi ni kwako wewe uliyejiandikisha na tume kama tume hatuna taarifa rasmi na kwa vile ni kinyume na taratibu basi nina hisi wengi wanapata tatizo hilo ni wale watu ambao hawafahamu jinsi ya kutunza kadi zao za kupigia kura – Tume ya Uchaguzi
Ikiwezekana kama utakuwa unaweza kunakili kadi namba ili kikipotea uweze kuripoti basi itakusaidia na unaweze ukaonekana pale kwenye kituo cha kupigia kura kwa kutumia busara  tume inataratibu ambazo zinaweza kumuwezesha mtu ambaye amepoteza kadi lakini yuko kwenye register kuweza kupiga kura‘ – Tume ya Uchaguzi
Lakini wewe hifadhi kadi yangu na hakuna kuitoa kwa mtu yoyote mpaka pale utakapoitumia siku ya kupiga kura tarehe 25 Octoba, 2015 kwahiyo hiyo kadi yako ni muhimu sana hakikisha isipote ili upate nafasi ya kupiga kura katika Uchaguzi huu 2015′ Tume ya Uchaguzi

Post a Comment