Bado Tanzania iko kwenye majonzi siku moja baada ya mazishi ya aliyekuwa mbunge wa Ludewa, Deo Haule Filikunjombe, Rubani Captein William Silaa na watu wengine wawili Egid Nkwera pamoja na Cassablanca Haule waliofariki kwenye ajali ya Helikopta kwenye mbuga ya Selous.
Taarifa iliyoingia kwenye vyombo vya
habari Kenya ni kuhusu Helicopter hiyo iliyopata ajali, imefahamika
ilikua ikimilikiwa na mwanasiasa maarufu wa Kenya ambaye pia ni mmoja ya
viongozi wa muungano wa vyama vya CORD pia makamu wa Rais kwenye
utawala wa Rais Mwai Kibaki, Kalonzo Musyoka.
Helicopter hiyo ilikua imekodiwa kuja Tanzania kutumika kwenye kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu.
Helicopter hiyo aina ya Eurocopter AS 350B3 Écureuil ilinunuliwa
na mwanasiasa huyo mwaka 2013 wakati wa shughuli za uchaguzi mkuu Kenya
na baada ya hapo alikuwa akiikodisha kwa watu mbalimbali mpaka October 15 2015 ambapo ilipata ajali na kuteketea kwa moto katika Mbuga ya Selous na kusababisha vifo vya watu wote wanne waliokuwemo.
Post a Comment