Ads (728x90)

Tabs

Page


  Mourinho hana utaratibu wa kubadilisha badilisja safu ya ulinzi – kawaida yake hutumia safu ile ile msimu wote. Nemanja Matic yupo nje ya fomu, sio yule tena asiyeruhusu ukuta wake kukutwa na madhara. Branislav Ivanovic amekuwa kivuli cha mchezaji aliyekuwa miaka kadhaa iliyopita. Mchezaji bora wa mwaka wa EPL Eden Hazard bado hajaonyesha kiwango chochote cha maana msimu huu. Mshambuliaji wao Diego Costa amekuwa butu tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita.
Lakini kuna kitu kimoja kwenye kikosi hiko ambacho kinachokosekana mpaka sasa kwenye timu ambacho kilikuwepo msimu uliopita -silaha ya Chelsea msimu uliopita: Cesc Fabregas.
 
Chelsea waliuanza msimu uliopita wakiwa na moto wa gesi. Ndani ya wiki kadhaa tu wakawa wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa na ilionekana wazi Mourinho alikuwa amepata kikosi kitakachoitawala EPL kwa muda mrefu. Diego Costa aliuwasha moto EPL na kuwa ndoto mbaya kwa mabeki na makipa wa ligi hiyo. Lakini, mwanaume aliyekuwa nyuma ya mafanikio yake kwa kutoa assista kwenye magoli hayo – alikuwa muhimu kama au zaidi ya Costa mwenyewe.
   Cesc Fabregas alirudi kwenye premier league baada ya kutoka kuitumikia klabu yake ya utotoni FC Barcelona. Kitendo cha kuhamia Chelsea kiliwakera mashabiki wa Arsenal na maneno ya kejeli hayakuwaisha midomoni. Fabregas alikuwa akitoa majibu yake uwanjani kwa kiwango bora katikati mwa eneo la kiungo la Chelsea. Combination yake na Diego Costa ilikuwa kama imeunganishwa na kifaa cha umeme. walikuwa kwenye ubora wao. Hata hivyo mwanzo wake kwenye umekuwa mbovu mno. Akitoa assist moja tu na hakuna goli alilofunga, kiwango cha Fabregas cha sasa hakilingani kabisa na msimu uliopita. Msimu uliopita alitoa assist 18 – jambo ambalo lilikuwa la kawaida kwa kiungo huyo wa zamani wa Arsenal.
 
Hivi sasa Fabregas anaonekana kuwa na msaada mdogo sana kwenye safu ya ushambuliaji ya Chelsea. Haishangazi kuona hata magoli ya Costa yamepungua kabisa. Hii sio mara ya kwanza kwa Fabregas kutuhumiwa kupotea dimbani. Hili lilikuwa jambo la kawaida kwa mashabiki wa Barca – alikuwa akiuanza msimu vizuri lakini raundi ya pili ya msimu anapotea. Ni rahisi kuamini kwamba hili jambo lilomtokea msimu uliopita. Ingawa kiwango chake kilikuwa bado kizuri kiasi cha kuweza kusaidia timu yake kutwaa ubingwa, lakini kiwango chake baada ya Christmass hakikuwa cha kuvutia kama ambavyo tunashuhudia hivi sasa katika miezi hii ya karibuni.   Msimu huu Chelsea haijaanza vizuri kama ilivyozoea. Labda kitu kinachomuokoa Fabregas na lawama ni kwamba wachezaji wote wanacheza chini ya kiwango.
Cesc Fabregas ilibidi awe moyo wa Chelsea kama alivyokuwa msimu uliopita. Hazard anaweza kuwa alichukua sica nyingi na kupewa uchezaji bora, lakini Chelsea siku zote imekuwa ikiundwa na safu ya kiungo imara na safu ya kiungo ambayo inaweza kuongoza mchezo. Fabregas ni aina ya kiungo ambaye anaweza kuamua mchezo akiwa kwenyw kiungo. Huku washambuliaji wakiwa wanapita mbele yake, yeye ndio mtu wa kutegemewa kuwalisha mipira ili kuwadhuru maadui. Mpaka kufikia hatua hii kwenye msimu Fabregas hatimizi majukumu yake ipasavyo. Tumeshashuhudia nini anaweza kufanya, tunafahamu nini tutegemes kutoka kwake. Ndio maana kiwango chake cha kinatupa swali: Yupo wapi The Real Fabregas?

Post a Comment