Msanii kutoka kundi la Tip Top
Connections Madee maarufu pia kwa jina la ‘Rais wa Manzese’ ambao ndio
wandaaji wa michuano ya Magufuli Cup #Hapa Kazi Tu amesema amefurahi
kutokana na mashindano hayo kuwa na mwamko mkubwa kwa kuwaleta watu
tofauti pamoja kwenye viwanja zinapopigwa mechi za michuano hiyo.
“Nimefurahi mwamko umekuwa mkubwa
kadri siku zinavyozidi kwenda mbele, viwanja vinajaa sana watu hamasa
imekuwa kubwa halafu tunazidi kuona vipaji ambavyo watu hawajaviona bado
na havijamulikwa na vyombo vikubwa”, amesema Madee.
“Kupitia Magufuli Cup tumewaona watu wengi na tunaamini baada ya hapa tutawasikia na kuwanaona kwenye ligi kubwa”.
“Mashindano yamekuwa magumu maana
hata hizo timu zilizofuzu hazijafuzu kirahisi, kwa mfano Abajalo na
Burudani zote zimefuzu kwa tofauti ya goli moja tu. Na toka tumeanza
mashindano haya hakuna timu ambayo imeshinda zaidi ya magoli matatu”.
Katika hatua nyingine Madee
anaipa nafasi timu ya Abaja kufanya vizuri kwenye michuano hiyo
kutokana na kuonesha kiwango kizuri kwenye mechi zake mbili za kwanza
dhidi ya Zakhem ambapo ilifanikiwa kushinda mchezo wa kwanza kwa goli
2-1 ikiwa kwenye uwanja wa Mwl. Nyerere kabla ya kutoka sare ya
kufungana kwa goli 1-1 kwenye uwanja wa Zakhem Mbagala.
Post a Comment