Ghasia za Jerusalem
Polisi wa
Israeli wanasema kuwa wamemuua kwa kumpiga risasi mwanamume Mpalestina
mjini Jerusalem baada ya kujaribu kuwashambulia.
Msemaji wa polisi anasema kuwa polisi walimkaribia mwanamume huyo kabla ya kumdunga kisu.
Hii ni kati ya misururu ya visa sawa na hivyo ambapo zaidi ya watu 40 wameuawa.
Waziri wa
mashauri ya kigeni nchini Marekani John Kerry amewapigia simu waziri
mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu pamoja na rais wa Palestina Mahmoud
Abbas na kuwataka kuleta utulivu.BBC
Post a Comment