Zilitoka ripoti kwamba Real Madrid wanaandaa pesa kwa ajili ya kumsajili mchezaji ambae anatoa msaada mkubwa kwenye kila ushindi wa Arsenal hivi sasa Alex Sanchez.
Real Madrid inasemekana wameshatenga fungu kwa ajili ya kupata huduma ya mchezaji huyu kwenye club yao. Sasa Sanchez amezungumza kwenye chombo cha habari na kujibu hizi tetesi.
“Nina furaha sana kwa sasa ndani ya Arsenal, sifikirii kuhama Arsenal kwa sasa. Siku zote nataka kufanya vizuri kwenye kila ninachokifanya, nafurai sasa hivi nafanya zaidi ya nilivyotaka kuonyesha siku zote.”.Haya ni maneno ya Alex Sanchez baada ya kuulizwa kuhusu tetesi za kusepa Arsenal na kujiunga na Real Madrid
Alex Sanchez mwenye miaka 26 ameshamaliza tetesi za yeye kutaka kujiunga na Real Madrid. Weekend hii Arsenal wanacheza na Watford na mechi hii inakujia Live kupitia Dstv pekee.
Post a Comment