Ni siku chache tu zimepita toka rappa na mfanyabiashara 50 Cent
aishangaze dunia na headlines zilizosema kuwa amefilisika, na badaae
kusema kwamba amefanya hivyo kulinda maslahi yake ya kiuchumi.
Headlines mpya kuhusu issue hii zimeanza kuibuka, jana 50 Cent alikuwa kwenye Mahakama ya Manhattan Supreme Court jijini New York kwa ajili ya kesi hiyo na amekiri mbele ya Mahakama hiyo kuwa vitu vingi alivyonavyo ni vya kukodisha na kukopesha.
Baadhi ya magazeti nchini Marekani yameripoti yakisema kuwa 50 amedai kuwa magari yake mengi yakiwemo ma-Lamborghini, Bentley na Rolls Royces alikuwa “ameyakodisha” na mikufu yake mingi ya dhabu aliipeleka ikayeyushwe na kutengenezwa upya ili ionekane mipya.
Jaji alipomuuliza kuhusu mauzo yake ya milioni 38 ya muziki, 50 Cent akasema anaingiza senti 10 kwa rekodi moja!
>>>“Ni
kama kwenye video za muziki, unaona vitu vingi vya thamani, magari
sijui mikufu na vitu kama hivyo…vyote hivyo hurudishwa kwa muuzaji, sina
changu pale…na sina thamani ya dola milioni 155 kama jarida la Forbes
linavyodai, thamani yangu halisi ni dola mil.4.4″. <<< 50 Cent.
Licha ya hayo 50 Cent amekubali kuingiza kiasi cha dola 100,000 (mil.200 za Tz) kutoka kwenye movie 2 alizoigiza, Spy na Southpaw hivi karibuni na dola 150,000 (mil.300 za Tz) kutoka kwenye series ya Power ambayo yeye ni executive producer.
Wewe unaonaje mtu wangu? 50 Cent kweli ana matatizo ya kiuchumi ama huu ni mpango tu wa yeye kukwepa ile faini ya dola milioni 5?
Post a Comment