Ads (728x90)

Tabs

Page


BRR2
Baada ya kuzuiliwa kutoka nchini Ufilipino kwa siku mbili hatimaye Chris Brown kaachiwa huru na kuondoka salama kabisa… msanii huyo ambaye alikuwa mjini Manila kwa ajili ya show alizuiliwa kuondoka siku ya Jumatano kutokana na madai ya kuwa hakutimiza wajibu wake wa kimkataba kipindi cha Mwaka mpya kuingia 2015.
Chris Brown performs at the Black Entertainment Television awards show
Licha ya kuachiwa huru Chris Brown alichukua time na kupost Twitter kusema hakuhusika na madai hayo na alitimiza wajibu wake wa kimkataba kwani alirudi kutoa show nyingine kufidia show aliyoikosa mwaka mpya.
>>> “Manila mmetisha sana, nawapenda sana…ishu iliyotokea sio ndogo na aliyehusika kufanya hivi inabidi atafutwe, jina langu limetumika na sikufanya CHOCHOTE!!”<<< Chris Brown.
BRR3
>>> “Sihusiki na hizi tuhuma, nilirudi Manila kufidia show niliyoikosa mwaka mpya..”. <<< Chris Brown.
Chris Brown ana show nyingine jijini Macau usiku wa July 24 2015 na kwenye video aliyoipost Twitter amewahakikishia mashabiki kuwa atakuwepo Live kwa ajili ya kutoa show hiyo.

Post a Comment