Unawakumbuka wale mashabiki wa Chelsea waliomshusha shabiki mwenzao kwenye treni ya Paris Metro kisa ana asili ya kiafrika?
Mahakana ya Stratford imewapiga marufuku kuhudhuria mechi za soka kwa miaka mitano ikiwa ni ugenini ama nyumbani.
Richard Barklie, kutoka Carrickfergus, Northern Ireland, Joshua Parsons pamoja na William Simpson wote kutoka Surrey wamepigwa marufuku kuhudhuria mechi baada ya mahakama kuridhika na adhabu hiyo.Jaji Gareth Branston alisema kwamba chuki ya kibaguzi ilionyeshwa na mashabiki wa Chelsea katika treni hiyo ya Paris na kuweza kiliharibu sifa soka ya Uingereza.
Ghasia hizo zilizuka wakati mashabiki wa Chelsea walipokuwa katika mji huo wa Ufaransa wakishabikia mechi ya klabu bingwa Ulaya kati ya Chelsea na Pasris Saint Germain tarehe 17 februari.
Baadaye kanda ya video iliibuka ikimuonyesha raia mmoja wa Ufaransa Souleymane Sylla akisukumwa nje ya treni na mashabiki hao.
Icheki video hapa…
Post a Comment