Babu Owino ni Kiongozi wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Nairobi,
aliwasilisha barua yake kwa Balozi wa Marekani ambaye yuko Kenya, ndani
ya barua kulikuwa na Ujumbe wa Wanafunzi wa Chuo hicho kwamba
wanahitaji Rais Obama akitua Kenya apitie na Chuoni hapo kwa ajili ya kuongea nao !!
Ratiba ikaonesha kwamba Rais Obama hatofika hapo… hawakupenda kwa sababu mwaka 2006 Rais Obama akiwa Senator wa Illinois alitembelea Chuoni kwao na akapanda mti wa kumbukumbu.
Kwenye barua ya wanafunzi hao ilionesha
kwamba wapo ambao wako tayari kujiua, wengine watajipanga kuukojolea
mti aliopanda mwaka 2006… Babu Owino alikutana na Rais Kenyatta na wakaongea kidogo tu kwamba hiyo haikuwa kitu kizuri kufanya kwenye ugeni mkubwa kama huu.
Mengine ni haya na yameshateka mitandao
ya Kenya tayari, wanafunzi wa Chuo Kikuu Nairobi wameuchoma moto mti huo
uliopandwa na Rais Obama, kuna mengine yatafuatia? Niko karibu na
updates za Nairobi kila wakati likinifikia jipya utalipata hapahapa mtu
wa nguvu.
Hapa iko video inayoonesha Babu Owino akiongea na Rais Kenyatta siku chache zilizopita.
Post a Comment