Baada ya dirisha dogo la usajili kwa Ligi Kuu soka Tanzania
bara kufungwa December 15, barani Ulaya ndio stori za usajili zinazidi
kuchukua nafasi. December 31 stori kutoka mtandao wa 101greatgoals.com
unaripoti klabu ya Arsenal ya Uingereza imekamilisha mipango ya usajili ya Mohamed Elneny.
Dirisha dogo la usajili kwa nchi za Ulaya linafunguliwa January 1 klabu ya Arsenal inaripotiwa kukamilisha mpango wa kumsajili Mohamed Elneny kutoka klabu ya Basel ya Uswiss kwa kumfanyia vipimo vya afya leo December 31, hivyo Arsenal tayari imeshatenga dau la pound milioni 7.3 kukamilisha dili hilo.
Arsene Wenger anatajwa kumsajili Mohamed Elneny staa wa Misri kutoka klabu ya Basel ili kuziba pengo la Santi Cazorla na Coquelin. Staa huyo wa Misri ambaye ana umri wa miaka 23, ameanza kuichezea timu ya taifa ya Misri toka mwaka 2011 na kucheza jumla ya mechi 39.
Post a Comment