Mshambuliaji wa kimataifa wa Mexico anayekipiga katika klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani Javier ‘Chicharito’ Hernandez, December 31 amerudi tena katika headlines za soka, baada ya mafanikio yake kuzidi kuonekana. Chicharito amerudi kwenye headlines baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi.
Kufuatia kushinda tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwezi, hii inatafsirika kama ishara aibu kwa kocha wa Man United Louis van Gaal
ambaye alisababisha kuondoka kwa mchezaji huyo, kutokana na kauli yake
ya kutompa nafasi ya kucheza na kumwambia kuwa hana nafasi katika kikosi
chake.
Chicharito aliyeondoka Man United
katika dirisha dogo la usajili la mwezi August 2015, ameshinda tuzo ya
mchezaji bora wa wezi mara mbili mfululizo, baada ya mwezi November
kufanikiwa kutwaa tuzo hiyo.
Kwa sasa Chicharito amecheza jumla ya mechi 14 akiwa na klabu ya Bayer Leverkusen na kufanikiwa kushinda jumla ya goli 11, wakati mshambuliaji tegemeo wa Man United Wayne Rooney ameshinda goli 2 katika mechi 15 alizocheza. Hii inadhiirisha kuwa Van Gaal alifanya makosa kumuacha Chicharito aondoke.
Post a Comment