Utafiti uliofanywa nchini Denmark umeonyesha uzani wa mwanamume huathiri seli za mbegu za kiume n...
Utafiti uliofanywa nchini Denmark
umeonyesha uzani wa mwanamume huathiri seli za mbegu za kiume na huenda
ukachangia katika kuwafanya watoto wanaozaliwa kuwa wanene
Seli za mbegu za kiume za wanaume wembamba na wanaume wanene zilikuwa na taarifa tofauti za kijenetiki, jambo ambalo huenda linaathiri utendaji wa chembe za kijenetiki.
Dkt Romain Barres, aliyesaidia katika utafiti huo alisema awali ilikuwa imebainika kwamba: “Mwanamke anapokuwa mjamzito anafaa kujitunza vyema. Lakini utafiti huu unaonyesha wanaume wanafaa pia kuangalia uzani wao.”
Utafiti huo ulifanywa kwa wanaume sita walionenepa kupindukia na ambao walikua wakisaidiwa kupunguza uzani. Watafiti walichunguza mbegu za kiume za wanaume hao kabla na baada ya kupunguza uzani baada ya mwaka mmoja.
Dkt Romain Barres mtafiti mkuu wa ripoti hii amesema waligundua tofauti iliyokuwepo kwa wanaume hao. Utafiti unasema kwamba zeli za mbegu za wanaume walionenepa husababisha mabadiliko ya tabia.
Aidha ripoti imeonya wanawake walio na mimba kuwa waangalifu sana hasa ikiwa walitunga mimba hizo wakiwa na wanaume walionenepa sana. Dkt Barres amesema wanaume walionenepa sana husababisha jeni zao kuanza kutamani kula chakula kila mara.
Ameongeza kwamba uzani wa mtu pia unaambatana na ukuaji wa akili. Utafiti huu uliochukua miaka mitano pia ulitofautisha wanaume 13 wenye uzani wa kadiri na 10 walionenepa zaidi. Hapo ikagunduliwa kwamba, wote walikua na tabia tofauti na zilizochochewa na mabadiliko ya seli kwenye mbegu za kiume.
Utafiti pia unasema uzani wa baba unaweza kusaidia, wanawe. Utafiti unasema kwa kula sana baba watoto pia huwahimiza wanawe kula sana ili wakue kwa haraka. Prof Allan Pacey amesema utafiti huu umebainisha kwamba baadhi ya tabia za watoto zimechangiwa na zilizokua mbegu za kiume za baba yao
Post a Comment