Morgan Shdneiderlin kujiunga na Man U japokuwa chaguo lake ni Arsenal
Midfielder kutoka nchini Ufaransa Morgan Schneiderlin ambae alikua kwenye list ya wachezaji wanaotakiwa na club kubwa za EPL kwa muda mrefu sana. Lakini huu ndio
umefika wakati wa yeye kujiunga na timu hizo. Taarifa za ndani kutoka kwenye gazeti la L’Equipe limeripoti kwamba uongozi wake umekubalina na Manchester ili yeye kuhamia kwenye club hiyo.
Inategemewa kutangazwa Jumatatu na mkataba utakua wa miaka 4. Kati ya Manchester united na Saints wamekubaliana malipo ya uhamisho wa €30m. Arsenal ilikua karibu pia kumsajili mchezaji huyu lakini imeshindika, pia inasemekana Arsenal ndio chaguo lake kubwa licha ya kujiunga na Manchester united. Kama tetesi hizi zikikamilika kama zilivyotufikia, Jumatatu mchezaji huyu mwenye miaka 25 atajiunga na Manchester united.
Hii ni video ya highlights zikionyesha ujuzi wa Morgan uwanjani
Post a Comment