Shirika la utafiti la saratani la WHO (IARC), limefanya uchambuzi wa
kitafiti wa jinsi matumizi ya nyama nyekundu iliyosindikwa kuwa
kisababishi cha saratani. Nyama iliyosindikwa ni ile iliyoongezewa
kemikali za kuifadhi isiharibike na yaweza kudumu kwa muda mrefu.
Lakini hii haimaanishi kuacha kula nyama kabisa, bali ni kuepuka nyama
zilizosindikwa mfano nyama za makopo. Ripoti hiyo inasema kuwa, ulaji wa
kadirio la gramu 50 za nyama iliyosindikwa itakuweka katika hatari ya
kupata
saratani ya utumbo mkubwa.
saratani ya utumbo mkubwa.
Nyama ni mojawapo ya kirutubisho muhimu chenye protini inayohitajika
kujenga mwili kwa hiyo hii haimaanishi kuacha kula nyama, bali kupunguza
matumizi ya ulaji wa nyama nyekundu pamoja na nyama zilizosindikwa.
Ripoti hii inatokana na ushahidi wa kitafiti na wa kisayansi
uliofanyika, na kulifanya shirika la afya duniani (WHO) kutoa tahadhari
ili kuwaepusha watu na maradhi haya hatari yanayotishia afya za watu
wengi ulimwenguni.
Post a Comment