Baada ya wiki ngumu Stamford Bridge, Chelsea wakianza vibaya huku pia Jose Mourinho akimuondoa katika benchi, daktari Eva Carneiro kwa madai ya kupoteza muda kwa kumtibia Eden Hazard, sasa Ex-boyfriend wa daktari huyo amefunguka na kusema yaliyojiri.
Mpenzi huyo wa zamani wa Eva, aitwaye Rupert Patterson-ward amesema aliachana na Eva kwa sababu alimwambia alikua akitembea na mchezaji mmoja klabuni hapo.
Rupert aliyekutana na Eva 2011 kabla hawaja achana 2013 anasema kwamba Eva ni mtu wa mapenzi sana na kwamba anapenda zaidi ngono.
Rupert anadai walitaka kufanya familia na kuoana lakini Eva alimfukuza na kumwambia kuwa alilala na mchezaji mmoja kikosini hapo.
Hata hivyo habari hizi hazina mahusiano ya moja kwa moja na kitendo cha Mourinho kumfukuza katika benchi mwanadada huyo.
Gazeti la Manchester Evening wiki hii liliripoti kuwa huenda Ivanovic akawekwa benchi kutokana na kuchukizwa na maamuzi ya Mourinho kumfukuza daktari huyo mrembo.
Hata hivyo wakitoa maoni wasomaji wa gazeti hilo, wamesema kila mtu ana haki ya kufanya mapenzi huku wakiamini inaweza pia kuwa mbinu za kumchafua Eva zinazofanywa na mpenzi wake huyo wa zamani.
Post a Comment