BAADA YA USAJILI MPYA….KIKOSI CHA CHELSEA KINAWEZA KUWA HIVI
Mourinho aliwai kusema kwamba yeye kwa msimu huu hatasajili kwa fujo anaamini kikosi chake kipo vizuri lakini mambo yanaonekana kuwa sio mambo kwake baada ya kuanza na dalili mbaya za kutetea ubingwa.
Sasa Chelsea wanafanya usajili wa haraka na kutumia pesa kadri iwezekanavyo ili wawe ndani ya muda na kuziba mapengo ya kikosi chao.
Chelsea imeshamsajili Baba Rahman ambae anategemewa kuwa pamoja Branislav Ivanovic kwenye defence ya Chelsea. Pedro anategemewa kuja kum-replace Oscar kwenye kikosi kitakachoanza akiwa pamoja Willian.
Baada ya kukatiliwa ofa yao kutaka kusajili John Stones, Chelsea bado haijakata tamaa na wanajiandaa kuweka mzigo mpya ili kumpata mchezaji huyu ambae anategemewa kujifunza mambo mengi kutoka kwa John Terry.
Wachambuzi wengi wanakipiga chapua kuwa hiki ndicho kikosi kinachoweza kuisaidia Chelsea kurudi kwenye harkati za kutete taji lake na sio kama walivyoanza.
Post a Comment