Ads (728x90)

Tabs

Page

Orodha ya wasanii wanaowania tuzo za All Africa Music Awards (AFRIMA) 2015 za Nigeria yametangazwa. Tanzania inawakilishwa na Diamond, Alikiba na upande wa wasanii wa kike ni Linah.
Wasanii wenye ushindani mkubwa Afrika Mashariki, Diamond na Alikiba pamoja na wasanii wenye ushindani mkubwa Afrika Magharibi, Davido na Wizkid wote kwa pamoja wamekutana katika vipengele muhimu vya ‘Wimbo Bora wa Mwaka’ na ‘Msanii Bora wa Mwaka’.

Alikiba na Diamond pia wanawania kipengele cha ‘Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki’, na Wizkid na Davido wanashindania ‘Msanii Bora Wa Kiume Afrika Magharibi’. Mwingine kutoka Afrika mashariki katika kipengele hiki ni Jose Chameleone wa Uganda.

Linah anawania kipengele cha ‘Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki’.
Upigaji wa kura umeanza August 14, na tuzo zitatolewa November 15, 2015 jijini Lagos, Nigeria.



Hii ni orodha ya Nominees.













Post a Comment