Ads (728x90)

Tabs

Page

gaal
Baada ya vyombo mbalimbali vya habari pamoja na baadhi ya wachambuzi wa soka nchini England kusema kwamba Manchester United inahitaji mshambuliaji mpya ili kumsaidia Wayne Rooney, kocha wa klabu hiyo mholanzi Louis Van Gaal haoni sababu ya kufanya hivyo.
Akizungumza mara baada ya mchezo wa timu yake na Newcastle United, uliomalizika kwa sare tasa isiyo na magoli, Van Gaal amesema timu yake ilionesha mchezo mzuri zaidi na kwamba walishindwa tu kutumia nafasi walizotengeneza.
Katika mechi hiyo, Manchester United walipiga mashuti sita golini katika dakika 20 za kwanza huku pia Rooney akikataliwa bao na mshika kibendera kwa madai ameotea.
Van Gaal amesema, haoni sababu ya kusajili straika mpya kwani timu yake ilifanya vizuri katika michezo dhidi ya Spurs, Aston Villa, Club Brugges na Barcelona pia katika michezo ya preseason.
Kuhusu Wayne Rooney, kocha huyo amemkingia kifua na kusem, “Wayne alifunga goli. Bahati mbaya lilikataliwa. Sihitaji mshambuliaji mpya” alijiamini Van Gaal.
Katika michezo mitatu ya ligi kuu England, Manchester United wameshinda miwili na kupata sare mechi moja huku wakifikisha points 7 na kufunga magoli 2 moja likiwa ni la kujifunga.
Hata hivyo wachezaji wengi wa Manchester United, wameonekana kuridhika na performance yao uwanjani, lakini wakasikitishwa na matokeo.
Wayne Rooney alikataliwa goli la mapema, huku kipa wa Newcastle mholanzi Tom Krul akimkatalia Javier Hernandez goli la wazi wakibaki wawili. Chris Smalling naye akagongesha mwamba akipiga kichwa mpira wa kona.

Post a Comment