Ads (728x90)

Tabs

Page

Mfupa ni sehemu ya mwili ambayo ina asilia ya ugumu husaidia kuupa mwili muonekano. Ndani ya mfupa huwa kuna kitu kinachoitwa Bone Marrow; Sehemu hii ipo katikati ndani ya mfupa ni laini ina  seli inayoitwa stem ambayo imeundwa na seli mbili seli nyeupe na seli nyekundu.
Kuna aina mbili za Bone Marrow
  • Bone Marrow nyekundu ambayo huweza kutengeneza damu
  • Bone Marrow ya njano ambayo haiwezi kutengeneza damu.
Seli nyekundu  hujaza karibia ya kila mfupa wa mtoto. Seli hizi huzalishwa ni tishu laini iliyopo ndani ya mfupa kwenye Bone Marrow inayoitwa Haemopoietic.
Mifupa ambayo huweza kuzalisha damu mwilini yaani yenye Bone Marrow ni uti wa mgongo, mfupa wa kwenye paja,mfupa ambao upo kwenye mkono unaotokea kwenye kiganja hadi kwenye kiwiko. fuvu,mbavu.
Nini kinaweza kuharibu sehemu hii ya kutengeneza damu kwenye mfupa?
  • Virusi mfano homa ya manjano, UKIMWI
  • Kuridhi
  • Ukosefu wa vitamini B12
  • Kansa
  • Kansa ya damu
  • Umri kadri umri unavyoenda marrow nyekundu hupungua kwenye mfupa kisha Marrow ya njano huongezeka.
Madhara ya kuharibu sehemu hii ya kuzalisha damu kwenye mfupa
  • Upungufu wa damu mwilini pale damu ikiwa chini ya 6g/dl
  • Kurudiarudia au kuumwa sana magonjwa yanayosababishwa Bakteria
  • Kuchubuka au kutoka damu kiraisi sehemu za fizi na pua.

Post a Comment