Historia ya Nelson Mandela ni historia ya kishupavu iliyosimamia ukweli, usawa na haki na pale mtu anapojaribu kuweka doa kwenye jina la familia ya Nelson Mandela watu hawatakuelewa kabisa.
Mjukuu wa Nelson Mandela, Mbuso Mandela mwenye miaka 25 anaziandika headlines South Africa baada ya kesi ya ubakaji wa msichana wa miaka 15 dhidi yake kufikishwa Mahakamani.
Kwa taarifa zilizotolewa na ripoti iliyofikishwa polisi zinasema kuwa Mbuso Mandela alimshambulia binti huyo wakati wakiwa kwenye restaurant moja maarufu jijini Johannesburg… na wakati akiwa anapata chakula cha jioni na marafiki zake msichana huyo aliinuka kwenda msalani ambako Mbuso alimfuata nyuma kumshambulia na kumbaka.
Mbuso alifikishwa Mahakamani siku ya Jumatatu jijini Johannesburg kusikiliza mashitaka hayo lakini polisi wamesema mjukuu huyo ya kiongozi mkubwa wa Africa ataendelea kushikiliwa na polisi mpaka tarehe yake ya kutolewa dhamana itakapotajwa.
Licha ya hayo, familia ya binti huyo imetoa malalamiko mengi dhidi ya familia ya Mandela huku wakidai aliyekuwa mke wa Nelson Mandela, Winnie Mandela
amekuwa akijaribu kwa kila njia kuipoteza kesi hiyo na ameshajaribu
zaidi ya mara moja kwa kumtumia bodyguard wake kujifanya kama polisi
kwenda kuiambia familia ya binti huyo kuwa Mbuso hawezi kushitakiwa wala kufungwa.
>>>“Eti
kwa sababu wana jina kubwa la ukoo wanahisi wanaweza wakafanya lolote
na wakakimbia. Watoto wetu hawawezi kubakwa tu alafu wategemee kila kitu
kiwe sawa, hapana huu ni uonevu”<<< nimenukuu kutoka kwa msemaji wa familia wa msichana huyo.
Kesi hiyo itasikilizwa tena siku ya Ijumaa wiki jijini Johannesburg South Africa.
Post a Comment