Ni kawaida ukikutana na warembo sikuhizi
wamependeza wenyewe, na simu zao wanataka zipendeze vilevile, basi kuna
cover za kila aina utawakuta nazo.. wengine midoli, wengine ni maua
maua… wanaume ni kawaida pia ukakutana na jamaa ana cover inaonekana
kama nguo ya kijeshi hivi.
Jamaa aliyeingia kwenye Headlines
Taiwan kakutwa na cover ya simu ambayo imekaa kama Bastola hivi, Polisi
wakamwita wakaanza kumhoji kuhusu hiyo kitu ambayo ilikuwa inaonekana
ameichomeka kwenye mfuko wa nyuma!!
Baada ya mahojiano Polisi wakagundua kwamba hiyo ni cover ya simu, wakamwachia.
Siku chache zilizopita aina hii ya cover
za simu iliingia kwenye headlines Marekani ambapo watu wa Usalama
walisema silaha sio kitu cha kuleta nacho utani, wameshuhudia mabalaa
mengi ya matumizi ya silaha kwa hiyo hawako tayari kuona cover hizi
zinazagaa mitaani na watu wanatumia!
“Zimeingizwa
sokoni na watu wanavutiwa nazo sana, ila zilipaswa kuwekwa lebo ya
‘HATARI’… Leo hii tunasema kwamba bastola sio kitu cha mchezo”—Hii ni nukuu ya alichokisema Chuck Schume, Senator wa New York Marekani.
Post a Comment