Ads (728x90)

Tabs

Page



shhhShilole amepost picha Instagram akiwa na Ommy Dimpoz wanajiandaa kwa ajili ya show Marekani… Shilole alifungiwa na BASATA kujihusisha na shughuli yoyote ya muziki, ikabidi 255 imtafute kujua mambo yakoje sasahivi?
Shishi anasema yeye si muongeaji wa hilo suala, liko mikononi mwa Mwanasheria wake ambae ni Albert Msando.
Shilole
Jana kichupa cha Juma Jux kilionyeshwa MTV, mwenyewe amesema anashukuru na kufurahi kuona muziki wake unafika mbali, anaamini itapokelewa na watu wengi zaidi na tofauti kwa wakati mmoja, pia imempa moyo zaidi wa kufanya kazi.
Anasema Video ya ‘Sisikii na ‘Nitasubiri’ aliwahi kuzipeleka lakini hazikupata nafasi, anaamini kazi zake ni nzuri lakini hajui kwa nini hazikuweza kupata nafasi kuchezwa kwenye TV kubwa.
juxxx
Jux
Wengi wanafahamu Diamond na Ali Kiba ni wasanii ambao hawana uhusiano mzuri, Diamond amefunguka na kusema yeye anafanya biashara na hawezi kuacha kufanya kitu chochote chenye manufaa kwake.
Diamond amesema yupo tayari kufanya kazi na mtu yoyote na hayupo kwa ajili ya kuweka beef na mtu, anatamani kumsapoti Mtanzania yoyote kwa moyo mweupe kabisa.
dd
Diamond

Post a Comment