Ads (728x90)

Tabs

Page

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Hosteli hizo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Picha na Ikulu.RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli ameagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kutumia Sheria zilizopo kuongeza kasi ya ukusanyaji wa madeni kwa wahitimu walionufaika na mikopo. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa hosteli za wanachuo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa gharama ya shilingi bilioni 10.
Amesema kuwa Serikali inadai takribani shilingi trilioni 2.6 kwa wahitimu walionufaika na mikopo ya Elimu ya juu.
“Serikali inawadai wahitimu walionufaika na mikopo ya Elimu ya juu takribani shilingi trillion 2.6 ambazo wanatakiwa kuzirudisha ili ziweze kutolewa kama mikopo kwa wanafunzi wapya na waliopo vyuoni” alifafanua Dkt Magufuli.
Aidha Dkt. Magufuli ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kusimamia ipasavyo suala la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi kwa kuzingatia vigezo vilivyopo kwani lengo la mikopo hiyo inawalenga watoto maskini.
Alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya malalamiko ya kuwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inafanya zoezi la ugawaji wa mikopo hiyo kwa upendeleo hivyo kuzitaka uongozi wa Wizara kushughulikia suala hilo.
Mbali na hayo Rais Magufuli amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kutimia mikopo hilo kwa malengo mazuri katika kujinufaisha na masuala ya Elimu.
Naye Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako alisema kuwa mradi wa ujenzi wa hosteli hizo utasaidia kuwahudumia wanafunzi 3,840 ambapo unatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwezi Desemba 2016.
Katika hatua hiyo Prof. Ndalichako alisema kuwa wanafunzi waliodahuiliwa kwa mwaka huu wapo 58,000 hivyo suala la wanafunzi 66,000 kukosa mikopo hiyo ni upotoshaji unaofanya na baadhi wa watu.
Mradi wa Ujenzi wa Hosteli za wanachuo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wenye majengo 20 kila jengo gorofa nne zenye vyumba 12 unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Desemba mwaka huu.

Post a Comment