Katika soka kila mchezaji huwa na jukumu
lake uwanjani, ataucheze vizuri vipi ila kama hutokuwa ukifanya vizuri
jukumu lako uwanjani, basi huwezi kuhesabika kama wewe ni mchezaji
mzuri, kwa maana ya kwamba kitu muhimu katika soka ni kumudu nafasi yako
uwanjani baada ya hapo ukiwa na vitu vya ziada watu watakupenda ila
kama nafasi yako uwanjani inapwaya halafu unaonekana kufanya vizuri nje
ya majukumu yako kamwe huwezi wekwa katika kundi la wachezaji bora.
Magolikipa ni watu ambao tumezoea
kuwaona wakikaa golini na jukumu lao kubwa ni kulinda goli ili
wasifungwe ila ikitokea golikipa akapiga chenga na kufunga goli basi
hiyo itakuwa ni uwezo wake wa ziada, November 15 2015 naomba nikusogezee
rekodi ya golikipa pekee aliyewahi kufunga hat-trick katika rekodi za
soka ambazo zipo katika kitabu cha Guinness.
José Luis Chilavert ndio golikipa pekee aliyewahi kufunga hat-trick katika soka, José Luis Chilavert alizaliwa Paraguay July 27 mwaka 1965 lakini amewahi kucheza soka katika vilabu kadhaa ikiwemo Real Zaragoza,
mwaka 1999 ndio aliweka rekodi hiyo baada ya kufunga magoli
matatu kupitia mikwaju ya penati, ilikuwa ni mchezo kati ya timu yake ya
Vélez Sarsfield dhidi ya Ferro Carril Oeste.
Rekodi ya José Luis Chilavert
haikuishia kufunga hat-trick pekee lakini yupo katika nafasi ya pili ya
rekodi ya muda wote ya magolikipa wanaoongoza kwa kufunga magoli mengi,
amefunga jumla ya magoli 62 nyuma ya golikipa wa kibrazil anayeongoza
rekodi hiyo Rogério Ceni anayeongoza kwa kuwa na jumla ya magoli 131. Kama ulikuwa hujui pia José Luis Chilavert ni mtaalam wa mipira ya faulo.
Video ya hat-trick aliyoifunga mwaka 1999
Post a Comment