Ni headline zilizotawala kwenye upande wa muziki wa bendi kuwa
mwimbaji na mnenguaji wa muziki wa densi nchini, Hassan Mussa aka Super
Nyamwela kuwa amerudi kwenye bendi yake ya zamani maarufu kama Twanga
Pepeta.
Sasa leo July 6, 2015 katika mahojiano na millardayo.com alifunguka na kusema ‘Kiukweli
kabisa mapokezi yalikuwa ni makubwa sana kwa watu ambao walikuwa
wamefika siku ambayo natambulishwa mimi ukumbi ulikuwa umejaa wengi
walikuwa hawaamini kuwa mimi na Choki tumerudi Twanga Pepeta lakini
nilivyofika pale na kutoa burudani wengi walivyofurahi kiukweli watu na
kuna watu ambapo nilikua sijawaona kama takribani ya miaka sita
niliwaona siku hiyo’- Super Nyamwela
‘Kwasasa maisha yetu sisi tunaonekana
kama vile kwamba wasanii ndio wanakuwa wanaama ama lakini sio sisi tupo
kwaajili ya kutengeneza maisha ya familia zetu kwa hiyo ikitokea bendi
nyingine siwezi kusema kwamba sitowezi kuhama kwasababu sio nadhili
lakini ikitokea bendi ambayo kabisa itanipa maslahi zaidi ya haya na
mimi nikaishi na familia yangu vizuri ambavyo ninavyotaka mimi
nitakubali kuhama nitaaga vizuri then mkataba ukiisha nitarudi nyumbani
kama kawaida‘- Super Nyamwela
‘Mimi nilikuwa katika bendi moja itwayo
Extra Bongo ambayo Choki alikuwa kama mkurugenzi na mimi nilikuwa kama
kiongozi wa bendi kwa hiyo imedumu mimi niliikutia katikati lakini
nimeweza kukaa kwenye bendi takribani ya miaka sita
Mimi nilikuwa naomba niwaambie mashabiki
kuwa mimi na choki tumerudi rasmi Twanga Pepeta ninahitaji support tu za
watanzania katika kazi zetu pia cha kumalizia naomba watanzania wawe na
uzalendo wa kuelewa nyimbo za wasanii wa ndani kisha zifuate za nje’- Super Nyamwela
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment