Zipo stori ambazo huwa zinazungumzwa na kubaki kwenye kumbukumbu za
Maisha yetu labda kutokana na kile ambacho uliamini kilikua sahihi kwa
wakati huo,Leo Mkongwe kwenye muziki wa
Bongo Fleva Prince
Dullysykes katufahamisha machache ambayo hatukuwa tukiyafahamu zaidi kutoka kwake.
Dullysykes ametumia sekunde 30 kuzungumza na
Clouds Fm kwenye
XXL kuwa miongoni mwa kazi ambazo ilikua afanye ni kwenda Jeshini>>’
Mimi
nilikuwa nataka kwenda Jeshi,ndiyo mwaka huo niliokuwa natoka sababu za
kutaka kwenda Jeshi ni utafutaji wa hela kuna kipindi nilikua nauza
viatu vya kike kwa kutembeza lakini maisha Mungu anapoamua kukupa kitu
anakupa,Mi namshukuru Mwenyezi Mungu amenipa kipaji cha muziki na kipaji
hiki kinanipatia mahitaji yangu sina kazi nyingine zaidi ya muziki‘.
Post a Comment